bpra banner

Kitengo cha usajili wa mali kinajumuisha usajili wa Tasnia ya mali za Ubunifu na Usajili wa Nyaraka mbalimbali zinazohusiana na mali zisizohamishika.


Usajili wa Tasnia ya Mali za Ubunifu


Usajili wa Tasnia ya Mali za ubunifu Zanzibar unasimamiwa na Sheria ya tasnia ya Mali za Ubnifu Nam. 4 ya mwaka 2008 (The Zanzibar Industrial Property Act No. 4 of 2008). Sheria hii imetungwa kwa lengo la kulinda haki zinazotokana na tasnia za mali za Ubunifu kwa kulingana na vigezo vya kimataifa.
Sheria hii inasimamia usajili wa Alama za Biashara (Trade and Service Marks), Hataza (Patents), Viashiria vya eneo (Geographical Indication), Hataza ndogo ndogo (Utility Models) na Tasnia za Maumbo (Industrial Design)

 

Alama za biashara na huduma


Alama za biashara maana yake ni alama yoyote inayoweza kuwasilishwa kimaandishi ambayo inaweza kutafautisha bidhaa (alama ya biashara) au huduma (alama ya huduma) ya biashara moja na zile za biashara nyengine. Alama inaweza kuwa ya maneno (pamoja na majina ya watu), maumbo, herufi, rangi au mchanganyiko wa rangi, nambari au umbo la bidhaa, sauti na harufu.

 

Mambo ya kuzingatia katika usajili wa Alama za Biashara


• Alama inayotaka kusajiliwa lazima iwe na uwezo wa kutafautisha bidhaa au huduma za kiwanda kimoja na zile bidhaa na huduma za viwanda vyengine.
• Alama inayotaka kusajiliwa isiwe kinyume na mwenendo au maadili ya jamii.
• Alama inayotaka kusajiliwa isiwe inaelekea kuupotosha umma au duru za kibiashara.
Namna ya kusajili Alama za biashara
• Ombi la usajili wa Alama za Biashara litawasilishwa kwa Mrajis na litajumuisha tamko la ombi, nakala ya Alama na orodha ya bidhaaau huduma ambayo inaombewa uandikishaji wa Alama inayohusika.
• Alama za Biashara zinazotakiwa kusajiliwa lazima ziwe zimeorodheshwa kwenye kundi au makundi (classes) muafaka ya utabakisho wa kimataifa.
• Ombi litatakiwa kulipwa ada iliyowekwa
• Gharama za usajili wa Alama wa Biashara
 Ada ya maombi (Application fee) Sh, 75,000/=
 Ada ya tangazo ya Alama ya Biashara (Advertisment fee) Sh. 15,000/=
 Ada ya usajili wa Alama ya Biashara (Registration fee) Sh. 75,000/=


Muda wa ulinzi wa Alama ya Biashara


• Alama ya biashara iliyosajiliwa italindwa kwa muda wa miaka kumi (10)
• Mmliki anaweza kuomba kuongezewa muda wa kuendelea na ulinzi wa alama ya biashara.
• Kipindi cha nyingeza ni miaka saba (7)
• Hakuna kikomo cha vipindi vya kuwekewa ulinzi