Firm Registration

Jina la biashara ni utambulisho wa biashara unaotumiwa na mfanya biashara pekee, ubia au kampuni, ambao hutofautiana na majina yao kibinafsi kwa lengo la kuendesha biashara kama taasisi ya biashara.  Sheria ya Majina ya Biashara inaweka masharti na mahitaji yanayohusu matumizi ya majina ya biashara na kutoa taarifa ya mahitaji ya baadhi ya maelezo juu ya umiliki.

Majina ya Biashara husajiliwa kwa Sheria ya Usajili wa Majina ya Biashara Sura ya 168 ya Sheria za Zanzibar.
Usajili wa jina la biashara hupitia hatua kuu nne:
(a) Kutafuta jina pamoja na kukugua fomu ya maombi.
(b) Kukubalika au kukataliwa maombi.
(c) Kufanya malipo ya usajili iwapo maombi yatakubaliwa.
(d) Utayarishaji wa nyaraka za usajili.

Jina la biashara linatakiwa liwe
• La kipekee (angalau katika eneo ambalo linatumika kibiashara)
• Lina jumuisha taarifa zote muhimu za kisheria.

Jina la biashara halipaswi kuwa na
• Matumizi ya maneno kinyume cha sheria au kukera (lisiwatenge watu kwa mtazamo wa biashara)
• Maneno ya matusi au yaliyopigwa

Mbali na maelekezo ya kisheria jina zuri la biashara linakuwa:
• Rahisi kulitamka na kulikumbuka.
• Linahisiana na aina ya biashara inayofanywa.
• Liwe na maana nzuri kwa wateja.

• Gumu – lisihitaji kutolewa maelezo kila wakati
• Utata – jina lenye utata wa maana linaweza kuwachanganya wateja
• Kuainisha misimu maalum – maeneo ya misimu yanaweza kuifanya biashara iwe nje ya mtindo kwa kasi.

1. Muombaji analazimika kujaza fomu ya maombi kwa ajili ya kusajili jina la biashara
• Kwa ajili ya watu binafsi, kujaza fomu no. 3
• Kwa ajili ya ushirikiano, ubia au shirika, kujaza fomu no. 2
2. BPRA inafanya ukaguzi wa jina kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria.
3. Kibali au kukataa maombi
Maombi ya kusajili jina la biashara yatakubaliwa tu iwapo masharti yaliyowekwa kwenye sheria ya usajili wa Majina ya Biashara yatafuatwa.

Fomu ya maombi Sh. 3,000/=
Ada ya usajli Sh. 30,000/=
5. Muombaji anakabidhiwa Hati ya Usajili na fomu ya dondoo (Extract Form) ambayo humuwezesha kufungua akaunti ya benki.

• Muombaji hujaza fomu kwa ajili ya maombi ya kubadilisha taarifa katika jina la biashara lilisajiliwa.
• Baada ya ada husika kulipwa, Hati ya madiliko hutolewa pamoja na fomu ya dondoo.

Kufuta matumizi ya Jina la Biashara
• Muombaji hujaza fomu ya kuacha kulitumia jina la biashara
• Kuambatisha na hati ya awali ya usajili
• Kulipa ada ya Sh. 5,000/=

USER GUIDE FOR ORSZ
Firm
Company
Documents
About Us
Contact Us
CONTACT US
USER GUIDE FOR ORSZ
Firm
Company
Documents
About Us
Contact Us

©2023 - Zanzibar Business and Property Registration. Developed by: CMB

Terms and Conditions / Privacy and Policy